Huduma ya Kuhamisha ofisi na makazi

LGV Movers tunatambua changamoto zilizopo wakati wa kuhama kutoka sehemu moja kwenda makazi mapya au ofisi mpya.

Baadhi ya changamoto hizo ni kuvunjika kwa vitu vya thamani kubwa na ndogo mfano; runinga(TV) na vinginevyo, kupotea kwa baadhi ya vitu, kuharibika kwa vitu mfano; samani kukwaruzika na kadhalika, zoezi zima kuchukua muda mrefu usio tegemewa na mengine mengi.

Hivyo basi tupo kwa ajili ya kukuhudumia na kukuepusha na changamoto hizo, ni jukumu letu kuhakikisha unapata huduma bora inayofanyika kwa ufanisi mkubwa na kukufanya mwenye amani huku ukiendelea na majukumu mengine wakati zoezi la kuhama likiendelea.

Tunafanya yafuatayo kuhakikisha unahama vyema na vitu vyako vinafika salama kwenye makazi mapya au ofisi mpya.

  1. 1. Tunafanya tasmini ya vitu vyote vinavyotakiwa kuhamishwa na kutoa gharama bure kwa mteja
  2. 2. Tunafanya shughuli zote sisi wenyewe kwa kutumia timu yenye watu wazoefu na wenye uweledi katika    shughuli ya uhamishaji.
  3. 3. Tunafungasha vitu vyote vinavyotakiwa kuhamishwa, tunavipakia kwenye gari zetu na kuvifikisha mahali husika, tunavitoa kwenye boksi na kuvipanga kwa kadri mteja anakavyo pendekeza.
  4. 4. Endapo kutakuwa na samani zinazohitaji kufunguliwa tutazifungua, tutazihamisha na kuzifunga upya mara baada ya kuzifikisha mahala husika.
  5. 5. Tunatumia vifaa maaluum kwa ajili ya kufungashia vitu mbalimbali ili kuhakiksha vinahamishwa salama pasipo kuvunjika, kuchunika, kuharibika wala kuchafuka. Mfano; Tunatumia boksi maalum kwa ajili ya uhifadhi na ubebaji, pia kwa vitu vya jikoni tunatumia karatasi maalum zinazozuia mikwaruzo,uchafu na uwezekano wa kuvunjika.
  6. 6. Tunaweka alama za kumbukumbu katika kila kitu ili kuepusha kuvichanganya na vitu vya sehemu nyingine wakati wa kuvipanga katika makazi /ofisi mpya.

Pia tunatambua uwepo wa virusi vya Corona, hivyo basi tunahakikisha tuko salama na wateja wetu wanabaki salama. Tunajikinga kwa kuvaa barakoa na kutumia sanitiza muda wote.

KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NASI KWA NAMBARI ZETU ZA SIMU AU BARUA PEPE
E-Mail: info@lgvmovers.com | Office Mobile: +255679495132 | Office Tel: +255222630753